ENGLAND wakiwa Uwanja wa kwao wa Nyumbani Wembley Jijini London wamecheza Mechi yao ya mwisho ya Kirafiki kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya EURO 2016 zinazoanza huko France Juni 10 na kuifunga Portugal 1-0.
Wakicheza bila ya Nahodha wao Cristiano Ronaldo aliepewa Mapumziko, Portugal walijikuta wakibaki Mtu 10 katika Dakika ya 35 baada ya Beki wao Mkongwe Bruno Alves kuinua Buti juu na kumkwangua kichwani Harryu Kane na Refa Marco Guida kutoka Italy kutoa Kadi Nyekundu.
Licha ya pigo hilo, Portugal walimaliza Kipindi cha Kwanza wakiwa 0-0.
Mechi hii ilielekea kutoka sare lakini Dakika ya 86 Sentahafu wa Manchester United aliipa ushindi England kwa Bao safi la Kichwa.
Huu ni ushindi wa 3 mfululizo kwa England katika Mechi zao 3 za maandalizi kuelekea EURO 2016 ambapo pia walizifunga Turkey na Australia 2-1 kila moja.
England wataanza EURO 2016 Juni 11 katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi B dhidi ya Russia na kisha kucheza na Wales na Slovakia huko France.
VIKOSI:
England: Hart; Walker, Cahill, Smalling, Rose; Dier, Alli, Milner; Rooney, Kane, Vardy.
Akiba: Forster, Sterling, Lallana, Clyne, Henderson, Sturridge, Stones, Wilshere, Barkley, Rashford, Heaton.
Portugal: Rui Patricio; Vieirinha, Bruno Alves, Carvalho, Eliseu; João Mário, Danilo Pereira, Adrien Silva, João Moutinho, Rafa; Nani, Rafa.
Akiba: Lopes, Fonte, Guerreiro, Eder, William Carvalho, Andre Gomes, Renato Sanches, Quaresma, Cedric, Eduardo
REFA: Marco Guida [Italy]
ENGLAND – Mechi zao:
Ratiba/Matokeo:
Mei 2016
Kirafiki
Jumapili Mei 22
England 2 Turkey 1
Ijumaa Mei 27
England 2 Australia 1
Juni 2016
Alhamisi Juni 2
England 1 Portugal 0
EURO 2016 Kundi B
Jumamosi Juni 11
2200 England v Russia
Alhamisi Juni 16
1600 England v Wales
Jumatatu Juni 2
2200 Slovakia v England


0 comments:
Post a Comment