MAN UNITED KUKAMILISHA DILI ZA MKHITARYAN NA IBRAHIMOVIC!

 

Manchester United wanakaribia kukamilisha Dili za kuwasaini kuwasaini Kiungo Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic.
 
Meneja Mpya wa Man United, Jose Mourinho, anaisuka upya Timu yake na tayari ashamchukua Beki wa Villareal Eric Bailly, Mchezaji wa Kimataifa wa Ivory Coast.



Dortmund wamekuwa wakimng’ang’ania Mkhitaryan aliebakiza Mwaka mmoja katika Mkataba wake lakini sasa inaelekea Ofa ya Pauni Milioni 30 ya Man United wataikubali.

Mkhitaryan, Raia wa Armenia, alijiunga na Dortmund kutoka Shakhtar Donetsk Mwaka 2013 kwa Pauni milioni 23.5.

Dili hii inatarajiwa kukamilika ndani ya Wiki moja.
 Zlatan Ibrahimovic, who will retire from the international scene after Euro 2016, is leading the way for Sweden

Nae Zlatan Ibrahimovic, ambae pamoja na Mkhitaryan Wakala wao ni mmoja, Mino Raiola, tayari ana Makubaliano ya Awali na Man United ikiwa pamoja na maafikiano ya Mshahara wake, anatarajiwa kukutana na Jose Mourinho Wiki hii.

Ibrahimovic ameondoka Paris St-Germain hivi Juzi baada ya kumaliza Miaka Minne ambapo alitwaa Ubingwa wa France mara 4 na sasa anatarajiwa kujiunga tena na Jose Mourinho ambae walikuwa wote huko Inter Milan Msimu wa 2008/09.

Hivi Juzi, Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, alitangaza kustaafu kuichezea Sweden ambayo ilitupwa nje hatua ya Makundi ya EURO 2016 bila yay eye kufunga hata Bao moja.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment