
WENYEJI France wakiwa huko Stade de France Mjini Paris Mjini Nchini wameitwanga Iceland 5-2 katika Mechi ya Robo Fainali ya mwisho ya EURO 2016, Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, na kutinga Nusu Fainali kwa kishindo.
Wakati France, kama Wenyeji, walitarajiwa kufika hatua hii, Iceland, Nchi ya Watu 330,000, haikutarajiwa kufika hapa lakini wamefika tena kwa kishindo baada ya kuitwanga England Mechi iliyopita katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kutoka nyuma kwa Bao 1 na kushinda 2-1.
Lakini Leo Iceland wamekiona cha mtema kuni na kufika kikomo chao kwa kunyeshewa mvua ya Magoli.
Bao za France hii Leo zilifungwa na Olivier Giroud, Bao 2 Dakika za 12 na 59, Paul Pogba, 19, Dimitri Payet, 42, na Antoine Griezmann, 45, wakati ya Iceland kufungwa Dakika ya 56 na Kolbeinn Sigthorsson na jingine Dakika ya 84 na Bjarnasson.
Kwenye Nusu Fainali hapo Alhamisi Julai 7 France watacheza na Germany ambao waliwatoa Italy Jana kwa Mikwaju ya Penati 6-5.
VIKOSI:
FRANCE: Lloris; Sagna, Umtiti, Koscielny [Mangala, 72'], Evra; Pogba, Matuidi. Sissoko, Griezmann, Payet [Coman 80'], Giroud [Gignacat 60’]
Akiba: Mandanda, Jallet, Cabaye, Gignac, Martial, Schneiderlin, Mangala, Digne, Coman, Costil
ICELAND: Halldorsson; Saevarsson, Arnason [Ingason 45'], Ragnar Sigurdsson, Skulason; Gudmundsson, Gunnarsson, Gylfi Sigurdsson, Birkir Bjarnason; Sigthorsson [Gudjohnsen 83'], Bodvarsson [Finnbogason 45']
Akiba: Kristinsson, Hauksson, Hermannsson, Ingason, Finnbogason, Sigurjonsson, Theodor Elmar Bjarnason, Magnusson, Hallfredsson, Traustason, Gudjohnsen, Jonsson
REFA: Björn Kuipers (Netherlands)
EURO 2016
Ratiba/Matokeo:
ROBO FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo
Alhamisi Juni 30
(Stade Velodrome, Marseille)
Poland 1 Portugal 1 [Dakika 120: 1-1, Penati: Poland 3 Portugal 5]
Ijumaa Julai 1
(Stade Pierre Mauroy, Lille)
Wales 3 Belgium 1
Jumamosi Julai 2
(Stade de Bordeaux)
Germany 1 Italy 1 [Dakika 120: 1-1, Penati: Germany 6 Italy 5]
Jumapili Julai 3
(Stade de France, Paris)
France 5 Iceland 2
NUSU FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo
Jumatano Julai 6
(Stade de Lyon)
Portugal v Wales
Alhamisi Julai 7
(Stade Velodrome, Marseille)
Germany v France
FAINALI
Jumapili Julai 10
**Saa 4 Usiku, Saa za Bongo
(Stade de France, Paris)
Portugal au Wales v Germany auFrance

0 comments:
Post a Comment