IBRA AMJIBU CANTONA: ‘SITAKUWA MFALME WA MANCHESTER, NITAKUWA MUNGU!’

Zlatan Ibrahimovic sealed his move to Manchester United this month after competing at Euro 2016 in France 

MCHEZAJI MPYA wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amejibu mapigo vizuri kwa Lejendari wa Klabu hiyo Eric Cantona ambae alidai ‘Kutakuwa na Mfalme Mmoja tu wa Manchester!’.

Malumbano hayo ya Mastaa Wawili hawa yalianza mara tu baada ya kuthibitika kuwa Ibrahimovic amesaini Man United na Cantona, ambae alipachikwa Jina la ‘Mfalme’ wakati akiichezea Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kumtumia Staa huyo wa Sweden ujumbe wa Video uliosomeka:
Ibrahimovic retired from international football after Euro 2016 but is preparing for his debut season in England 
 “Nina ujumbe binafsi kwa Zlatan. Umeamua kuwa United na huo ni uamuzi sahihi ambao umewahi kufanya. Lakini kitu kimoja cha mwisho, kwa Manchester Mfalme ni mmoja tu. Unaweza kuwa Mwana wa Mfalme na Jezi Namba 7 ni yako ukiipenda. 

Ni zawadi yangu kwa kukukaribisha wewe. Mfalme ameondoka, Ishi Maisha Marefu Mwana wa Mfalme!”  

Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, akiongea na Gazeti la kwao Sweden, Aftonbladet, alisema: “Namhusudu Cantona na nimesikia alichosema. Lakini sitakuwa Mfalme wa Manchester. Nitakuwa Mungu wa Manchester!”\

Kauli hiyo, ambayo ilichukuliwa ni ya dhihaka, ilitolewa na Ibrahimovic wakati yuko Vakesheni huko Marekani na anatarajiwa kwenda Jijini Manchester Wiki hii kuanza rasmi Mazoezi na Wachezaji wenzake kwa ajili ya Msimu mpya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment