IVO MAPUNDA ALICHEZEA TIMU ZOTE KATIKA ‘DAR DERBY,’ SASA ANATUA KWA MAHASIMU WA GOR MAHIA

ivo-mapundaa
GOLIKIPA namba moja wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na vilabu vya Tanzania Prisons, Moro United, Yanga SC, St.George ya Ethiopia, African Lyon, Gor Mahia, Simba SC, Ivo Mapunda atajiunga na klabu ya ligi kuu ya Kenya, AFC Leopards kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Ivo mshindi wa mataji ya Ligi kuu Bara, ligi kuu ya Ethiopia aliisaidia Gor Mahia kushinda ubingwa wake wa kwanza baada ya kusubiri kwa zaidi ya muongo mmoja mwaka 2013. Alijiunga na Simba na kucheza hadi katikati ya mwaka uliopita baada ya misimu miwili na nusu.
Msimu uliopita alisajiliwa na Azam FC huku malengo mengine makubwa yakiwa ni kuwapa uzoefu makipa Aishi Manula na Mwadini Ally.
Baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mwaka mmoja katika timu ya Azam wengi walidhani kipa huyo aliyedumu kwa miaka 16 katika ligi za juu atastaafu lakini badala yake anakwenda kutengeneza rekodi yake nyingine kwa kuzichezea timu zote nne kubwa zaidi katika Afrika Mashariki.
Leopards na Gor ni timu hasimu zaidi nchini Kenya huku pambano baina yao likitazamwa kama ‘pambano hatari’ zaidi nje ya uwanja huku masuala ya ukabila yakitajwa kuchangia uhasama mkubwa wa timu hizo za Nairobi.
Mapunda alicheza kwa wasiwasi mkubwa dhidi ya Simba wakati alipokuwa Yanga, lakini alikuwa mchezaji kiongozi mzuri wakati akiidakia Simba katika ‘Dar es Salaam derby.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment