Hawa
wawili ni wapinzani wakubwa, Jose Mourinho na Pep Guardiola, lakini ni
uwanjani. Nje ya uwanja ni watu wanaofahamiana maana walifanya kazi
pamoja katika kikosi cha Barcelona, Mourinho akiwa kocha msaidizi na
Guardiola akiwa mchezaji, tena nahodha.
Baadaye
wakaonyeshana kazi mmoja akiwa Real Madrid na mwingine FC Barcelona.
Sasa Mourinho yuko Man United na Guardiola yuko Man City, upinzani
unaendelea.
Mourinho
safari hii ilikuwa ni zamu yake ya ushindi, ameshinda kwa bao 1-0 dhidi
ya Guardiola, hakuna ubishi, soka raha sana, hasa ukiwa hauna hasira.

0 comments:
Post a Comment