
MECHI za Raundi ya 10 ya Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka Nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia zimeendelea Alfajiri hii na Vinara Uruguay kushushwa toka kileleni na Brazil wakati Argentina ikitandikwa Nyumbani kwao.
Wakicheza Ugenini huko Estadio Olímpico Metropolitano de Mérida, Mérida, Brazil waliwafunga Wenyeji Venezuela 2-0 kwenye Mechi iliyosimama kwa Dakika 10 kuanzia Dakika ya 75 baada ya Taa za Uwanjani kuzimika.
Bao za Brazil, waliocheza bila Kepteni wao Neymar ambae yuko Kifungoni kwa Mechi 1, zilifungwa na Gabriel Jesus, Dakika ya 8, na Willian, Dakika ya 53.
Nao Uruguay walitoka 2-2 na Colombia kwenye Mechi iliyochezwa huko Uruguaya huku Bao za Wenyeji hao zikifungwa Dakika za 27 na 73 na Rodriguez na Luis Suarez huku za Colombia zikipigwa Dakika za 15 na 84 na Aguilar na Mina.
JE WAJUA?
-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.
Nao Argentina, wakicheza Ugeni huko Lima, Peru bila Staa wao Lionel Messi walifungwa 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Derlis González.
Baada ya Mechi 10 kwa kila Timu, Brazil ndio wanaongoza wakiwa na Pointi 21 wakifuata Uruguay wenye 20, kisha Ecuador na Colombia zikiwa na 17 kila mmoja na Aregentina ni wa 5 wakiwa na Pointi 16.

VIKOSI:
VENEZUELA (Mfumo 4-2-3-1): Hernandez; Rosales, Angel, Velazquez, Feltscher; Rincon, Flores; Martinez, Anor, Penaranda; Rondon
Akiba: Farinez, Figuera, Murillo, Contreras, Garcia, Villanueva, Herrera, Ponce, Guerra, Del Valle, Chancellor, Otero.
BRAZIL (Mfumo 4-3-3): Alisson; Alves, Marquinhos, Miranda, Luis; Renato, Fernandinho, Paulinho; Willian, Coutinho, Gabriel
Akiba: Firmino, Lima, Fagner, Weverton, Carioca, Taison, Alex, Gil, Silva, Giuliano, Oscar, Wendell.
REFA: Victor Carrillo [Peru]
MSIMAMO:
CONMEBOL
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Ratiba:
**Saa za Bongo
CONMEBOL
Jumanne Oktoba 11
2300 Bolivia v Ecuador
2300 Colombia v Uruguay
Jumatano Oktoba 12
0230 Chile v Peru
0230 Argentina v Paraguay
0330 Venezuela v Brazil

0 comments:
Post a Comment