
MTANANGE wa EPL, Ligi Kuu England wa Mahasimu wa Jadi huko England, Liverpool na Manchester United, utachezwa Anfield Jijini Liverpool Jumatatu Oktoba 17 na tayari mgogoro ushaanza kufukuta baada ya uteuzi wa Refa wa Mechi hiyo kubainika ni mkazi wa Jiji la Manchester Nyumbani kwa Manchester United.
Professional Game Match Officials Limited (PGMOL), Mamlaka inayosimamia Marefa wa Gemu za Kulipwa, imemteua Anthony Taylor, mwenye Miaka 37 na anaetoka Kitongoji cha Wythenshawe kilichopo Maili 6 tu toka Old Trafford Nyumbani kwa Man United huko Jijini Manchester, kuwa Refa wa Mechi hiyo.
Keith Hackett, Refa wa zamani na Mkuu wa zamani wa PGMOL, amezungumzia uteuzi wa Refa Anthony Taylor na kusema kutaibuka malamiko makubwa ikiwa Refa huyo atafanya kosa lolote kwa upande wowote ule.
Mwezi Aprili Mwaka huu, Refa Kevin Friend aliondolewa kuchezesha Mechi ya Tottenham Hotspur na Stoke City baada ya kuibuka dhana ya Refa huyo kuisapoti Leicester City ambayo wakati huo ilikuwa ikichuana vikali na Tottenham kutwaa Ubingwa wa England ambao hatimaye ulitwaliwa na Leicester City.
Mwaka 2014, Meneja wa Liverpool wakati huo, Brendan Rodgers, alipigwa Faini na FA, Chama cha Soka England, baada ya kulaumu uteuzi wa Refa Lee Mason kusimamia Mechi na Manchester City huko Etihad Stadium ambayo walifungwa 2-1.
Brendan Rodgers alidai: “Nilishangaa tunacheza Jijini Manchester na Refa anatoka Jijini Manchester! Natumaini Siku zijazo hatutakuwa na Refa wa Jijini Manchester kuchezesha Mechi ya Liverpool dhidi ya Manchester United!”
EPL - LIGI KUU ENGLAND
Saa za Bongo
Jumamosi 15 Oktoba 2016
1430 Chelsea v Leicester City
1700 Arsenal v Swansea
1700 Bournemouth v Hull
1700 Man City v Everton
1700 Stoke v Sunderland
1700 West Brom v Tottenham
1930 Crystal Palace v West Ham
Jumapili 16 Oktoba 2016
1530 Middlesbrough v Watford
1800 Southampton v Burnley
Jumatatu 17 Oktoba 2016
2200 Liverpool v Man United

0 comments:
Post a Comment