Pointi 3 kutoka Mbao FC zaendelea kuiweka Simba kileleni VPL



img_4542
Goli pekee la Muzamiru Yassin dakika ya 86 limeipa Simba pointi tatu nyingine kwenye uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam wakati wakipambana na timu iliyopanda ligi msimu huu Mbao FC kutoka jijini Mwanza.
Licha ya ugeni wao kwenye ligi, Mbao FC ambao wamepanda ligi kuu msimu kwa mara ya kwanza waliweza kuhimili vishindo vya wakongwe wa ligi hiyo Simba na kuchelewesha ushindi wao hadi dakika ya 86.
Blagnon ambaye aliingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo, alitoa pasi ya goli kwa Mzamiru Yassin ambaye alikandamiza mpira nyavuni na kufunga bao lake la pili tangu ajiunge na Simba.
Mzamiru alifunga goli lake la kwanza ndani ya uzi wa Simba kwenye mechi iliyopita wakati Simba ilipocheza dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment