Post ya Nay wa Mitego kuhusu Wema Sepetu na Milioni 500 za Idris

Nay wa Mitego ni kati ya Mastaa wa Tanzania ambao karibia kila wanachokifanya kwenye maisha yao hugeuka kuwa Headlines kubwa kutokana na style ya vitu wanavyofanya. Leo October 27, 2016 kupitia Instagram Rapa Nay wa Mitego a.k.a True Boy amepost video mbili akiwazungumzia Wema Sepetu na Idris Sultan.
Kwa mujibu wa Video hizo Nay anasikika akihoji kilichomaliza pesa za mshindi huyo wa shindano la Big Brother Afrika msimu wa 2014 na kuondoka na mkwanja mrefu sana kiasi cha shilingi Milioni 500.
Baada ya ushindi wake Idris aliingia kwenye headlines za kudate na mastaa wengine akiwemo mshiriki mwenzake wa shindano la BBA Samantha ambaye waliachana na akaanza kudate na Wema Sepetu ambaye naye ziko stori kwamba wawili hao hawako pamoja japo hakuna aliyethibitisha wala kukanusha mpaka sasa.
Sasa Nay wa Mitego anauliza je zile Milioni 500 za Idris ni mwanamke gani amezimaliza kati ya Wema Sepetu au Samantha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment