Usiku wa October 20 2016 klabu ya
KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa
Stars Mbwana Samatta ilishuka katika uwanja wake wa Luminus Arena
kucheza mchezo wake wa tatu wa Europa League dhidi ya Athletic Bilbao
ya Hispania.

KRC Genk ambao tayari walikuwa
wanaongoza msimamo wa Kundi F kwa tofauti ya magoli ya kufunga na
kufungwa, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ya Genk
yakifungwa na Jakub Brabec dakika ya 40 na Wilfred Ndindi dakika ya 83.

Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta
aliingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya nahodha wao Thomas Buffel, kwa
sasa Mbwana Samatta anakuwa kaichezea Genk katika Europa League hatua ya
Makundi kwa jumla ya dakika 126, mechi ya kwanza alicheza kwa dakika
77, ya pili 15 na 34.

0 comments:
Post a Comment