Cristiano Ronaldo ameamua kujiweka kwa model wa Madrid


ronaldo-paris

Jarida la udaku la Italia linalofahamika kwa jina la Chi limezifuma picha mpya za superstar wa Madrid Cristiano Ronaldo akiwa amerejea tena kwenye game ya mahusiano.
Hivi karibuni Ronaldo alimwagana na Miss Spain wa zamani Desire Cordero, na inaokena ameamua kuendelea na maisha yake ya mahusiano na mtu mwingine.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno ameonekana akiwa kwenye mahaba mazito na mwanadada Georgina Rodriguez anayeishi pia katika jiji la Madrid.
Ronaldo alijaribu kuziuia asipigwe picha na mapaparazi lakini hakufanikiwa katika hilo baada ya picha zake kunaswa.
Cristiano aliamua kutupia kitu cha wig kichwani pamoja na capelo zinazovaliwa kwenye mchezo wa baseball pamoja na miwani ya jua (sunglasses) ikiwa ni mbinu za kujaribu kukwepa lens za camera lakini kwa namna picha zinavyoonesha ni kwamba jaribio lake lilifeli.
Jarida la Chi liliotea bonge la picha wakati Ronaldo aki-enjoy busu la mpenzi wake Georgina Rodriguez walipokuwa kwenye mtoko wao jijini Paris.
ronaldo-paris-1
Tetesi zinaonesha namna ambavyo Ronaldo aliweza kukutana na kifaa hicho kupitia mitandao ya kijamii.
Fununu zilizopo zinaeleza kwamba, wawili hao walikutana kwenye event ya D&G huku ikielezwa Ronaldo kuanza kumpeleka Santiago Bernabeu siku za hivi karibuni.
Baadhi ya picha kutoka kwenye account ya Instagram ya mlimbwende Georgina Rodriguez
Cristiano Ronaldo dates Georgina Rodriguez in a disguise. He gets caught
Cristiano Ronaldo dates Georgina Rodriguez in a disguise. He gets caught
Cristiano Ronaldo dates Georgina Rodriguez in a disguise. He gets caught
Cristiano Ronaldo dates Georgina Rodriguez in a disguise. He gets caught
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment