KRC Genk imefuzu hatua ya mtoano Europa League


karelis
Ushindi wa bao 1-0 iliopata KRC Genk dhidi ya Rapid Wien unaipa nafasi timu hiyo inayotumikiwa na Mbwana Samatta kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano ya Europa League msimu huu.
Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji raia wa Ugiriki Nikolaos Karelis dakika ya 11 tangu mchezo kuanza.
Nahodha wa timu ya taifa ya Taifa Stars Mbwana Samatta, aliingia uwanjani dakika ya 84 akitokea benchi kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao Nikolaos Karelis.
Matokeo hayo yanaifanya KRC Genk kufikisha jumla ya pointi 9 baada kucheza mechi 5 za Kundi F na kuongoza kundi hilo kwa tofauti ya magoli mbele ya Athletic Bilbao ambao wanalingana kwa idadi ya pointi na mechi walizocheza.
kundi-f-europa-league
Genk inasubiri kucheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi itakayoamua timu ipi itaongoza Kundi F wakati Sassuolo na Rapid Wien zenyewe zikisubiri kukamilisha ratiba kwasababu tayari zimeshatupwa nje ya mashindano hayo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment