Jamii ya wapendasoka ulimwenguni kote wameonekana kuguswa na ajali ya
ndege iliyohusisha timu ya Chapecoense ambayo imetokea usiku wa
kuamkia leo.
Ndege hiyo
iliyoanguka njiani ilikuwa imebeba klabu hiyo ya nchini Brazil kuelekea
Colombia kwaajili mchezo wao mkondo wa kwanza wa michuano ya Copa
Sudamericana dhidi Atletico Nacional.
Timu hiyo ilikuwa
icheze kunako dimba la Estadio Atanasio Girardot huko Medellin kesho
Jumatano lakini ndege yao iliyokuwa ina abiria takriban 72 ilianguka
njiani ikiwa Medellin wakati inatoka Santa Cruz de la Sierra huko
Bolivia, na kubakisha watu watano tu wakiwa salama.
Mamlaka mbalimbali
zimeripoti kuwa maafisa wa ndege hiyo walitangaza hali ya hatari majira
ya 22.00 kwa saa za huko baada ya kukumbwa na matatizo ya kiufundi.
Ndege hiyio inasadikiwa kuanguka maeneo ya Cerro Gordo huko manispaa ya La Union
Wanandinga
mbalimbali katika ulimwengu wa soka wameamua kutumia akaunti zao za
mitandao ya kijamii kutoa pole kutokana na janga hilo la Chapecoense.


0 comments:
Post a Comment