
Manchester United imeendelea kupata wakati mgumu kwenye michezo yake ya ligi kuu England baada ya kulazimisha sare nyingine ya kufungana goli 1-1 ugenini ilipocheza dhidi ya Everton kwe nye uwanja wa Goodson Park.
Zlatan Ibrahimovic aliiweka mbele Man United kwa goli lake la dakika ya 42 lakini Baines akaisawazishia Everton kwa mkwaju wa penati.
Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini alisababisha penati dhidi ya timu yake ya zamani kisha Leighton Baines akaisawazishia Everton kwa mkwaju wa penati katka dakika za lala salama.
Fellaini aliingia dakika ya 85 alimfanyia madhambi Idrissa Gueye ndani ya box ambapo Baines hakufanya makosa akiwa miguu 12 kutoka kwa golikipa.

- Baines amefunga penati 17 kati ya 19 ndani ya EPL sawa na asilimia 89.
- Phil Jagielka ametoa penati nyingi hadi sasa msimu (3) kuliko Fellaini kwenye mechi za Premier League.
- Anthony Martial ametoa assist ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu.
- Hakuna mchezaji yeyote aliyefunga magoli mengi akiwa nje ya box kuliko Ibrahimovic (Xherdan Shaqiri na Philippe Coutinho pia wamefunga magoli 3 kila mmoja).
- United wameshinda mchezo moja kati ya michezo yao nane iliyopita ya Premier League, wamepata sare sita na kupoteza mchezo mmoja.

0 comments:
Post a Comment