VIDEO: Ushindi wa AFC Bournemouth dhidi ya Liverpool Goldsands Stadium

Ligi Kuu England inaendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa, wakati unasubiria mchezo wa Everton dhidi ya Man United, timu ya Liverpool ikiwa ugenini katika uwanja wa Goldsands imecheza dhidi ya wenyeji wao AFC Bournemouth.
3b06f8ec00000578-3998682-image-a-17_1480861698425
Kama ni shabiki wa Liverpool najua utakuwa umesikitishwa na goli la dakika za lala salama la AFC Bournemouth lililofungwa dakika ya 90 ya mchezo na kuifanya Liverpool kutoka uwanjani vichwa chini kwa kufungwa jumla ya goli 4-3.
screen-shot-2016-12-04-at-7-00-59-pm
Magoli ya AFC Bournemouth yalifungwa na Callum Wilson dakika ya 56 kwa penati, Ryan Fraser dakika ya 76, Steve Cook dakika ya 79 na Nathan Ake dakika ya 90, huku Liverpool walianza kupata goli mapema tu dakika ya 20 kupitia Sadio Mane, Divock Origi dakika ya 22 na Emre Can dakika ya 64.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment