CONFIRMED: Usitarajie kumuona tena Sadio Mane katika EPL msimu huu


Baada ya taarifa za awali kutolewa na Liverpool kuwa kujulikana kwa hatma ya staa wao wa soka wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane kama ataweza kurudi uwanjani mapema au kumaliza msimu nje ya uwanja itajulikana baada ya saa 48 leo imetolewa taarifa rasmi.
Leo April 7 2017 taarifa iliyotolewa kuhusu Sadio Mane kutoka kwa kocha wa LiverpoolJurgen Klopp amesema kweli Sadio Mane anahitajika kufanyiwa upasuaji baada ya kushindwa kumaliza game ya jumamosi iliyomalizika kwa Liverpool kushinda kwa goli 3-1 dhidi ya Everton.
Mane aliyejiunga na Liverpool akitokea Southampton kwa dau la pound milioni 34, atazikosa mechi 7 za Liverpool za kumalizia msimu wa EPL baada ya kuthibitika kuwa atafanyiwa upasuaji wa goti, kabla ya kuumia Mane msimu huu amezikosa mechi 5 tu ambazo kati ya hizo tatu walitoa sare na mbili walipoteza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment