Ni juzi tu Zlatan Ibrahimovich amerejea uwanjani baada ya kutumikia kifungo cha michezo mitatu nje, Zlatan alipatikana na hatia baada ya kumchezea vibaya Tyrone Mings wakati wa mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Fc Bournamouth mwezi uliopita.
Kama unakumbuka tukio la Zlatan Ibrahimovich muamuzi hakuliona, sio muamuzi wa kati tu bali hata wa pembeni lakini picha za video zilimkuta na hati na hivyo FA kumchukulia hatu mshambuliaji huyo.
Sasa katika mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City kuna tukio lilitokea, mshambuliaji wa Chelsea Dieogo Costa lionekana akimpiga teke kwa makusudi beki Vicent Company wa Chelsea lakini Costa hakupewa kadi nyekundu.
Picha za video zilionesha wazi wazi tukio lile, na sasa kama ilivyokuwa kwa Zlatan Ibrahimovich inaweza kutokea pia kwa Costa, Costa anaweza kufungiwa kucheza michezo mitatu endapo FA watamkuta na hatia.
Hili linaweza kuwa pigo kwa Chelsea ambao wapo katika mbio za ubingwa, Costa ameshafung magoli 17 hadi sasa na kukosekana kwake katika timu hiyo kunaweza kupunguza kasi ya ufungaji katika kikosi hicho cha Antonio Conte.


0 comments:
Post a Comment