
Daily Mirror. Real Madrid wanaamini kabisa watamchukua Hazard kutoka Chelsea katika dirisha lijalo la usajili. Atletico Madrid wako njiani kumpa Antoine Griezman dili kubwa ili kumbakisha asiende Manchester United. Manchester City wako mbioni kumsajili winga wa Barcelona Marc Cucurella ambaye bado hajapewa mkataba na Barcelona. Baada ya kukaa kwa muda mrefu Arsenal wameamua kumpa mkataba Marcelo Allende aliyekuwa katika timu hiyo kwa majaribio.
Daily Mail. Katika kile kinachoonesha kuzikatisha tamaa timu za China, Uingereza na Ufaransa, mwenyekiti wa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Hans Joachim amesema mahambuliaji wao Pierre Aubemayang atazingatia ofa kutoka klabu mbili tu duniani ambazo ni Barcelona na Real Madrid.
The Sun. Pamoja na kwamba Chelsea na Juve ndio zinaongelewa sana kumtaka Sanchez lakini ripoti kutoka Sun zinadai Manchester City ndio wanaongoza katika mbio hizo. Mlinzi wa Napoli Elseid Hysaj anasakwa sana na vilabu vya nchini Uingereza, Arsenal na Manchester United wanaongoza katika mbili hizo.
Daily Star. Katika kuonesha kuchoshwa na kuburuzwa, klabu ya Arsenal imeamua kufanya usajili mkubwa, imeelezwa kwamba Arsenal nao wako kwenye mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez ambaye nafasi yake katika klabu hiyo ni finyu.
Daily Teleghraph. Baada ya kumtoa mtoa kwa mkopo sana, sasa klabu ya Manchester United imeamua kuanza kusikiliza ofa zitakazoletwa na vilabu vinavyomtaka Adnan Januzaj.

0 comments:
Post a Comment