
Baado United wanaonekana kusuasua, sehemu ya ushambuliaji ya timu hiyo haionekani kuwa na kasi kama ilivyotarajiwa, lakini matukio haya 5 yanaonesha jinsi United walivyo butu katika ufungaji.
1.Hary Kane, Delle Alli na Son Min wana magoli mengi kuliko Manchester United. Kwa pamoja Kane, Alli na Min wamefunga magoli 46 huku Kane akiwa na 19, Alli 16 na Min 11 lakini timu nzima ya Manchester United hadi sasa wamefunga jumla ya magoli 46.
2.Middlesbrough na Southampton tu wenye umaliziaji hafifu kuliko United. Ni aibu kwani timu yenye wachezaji wakubwa na wa gharama lakini takwimu inaonesha katika upigaji wao mashuti msimu huu wastani wao wa umaliziaji ni 12.2 huku Southampton na Middlesbrough ndio timu pekee zilizo chini ya United ambazo zina wastani mdogo wa umaliziaji nafasi wanazopata.
3.Swansea na Burnley wana magoli mengi nyumbani kuliko United. Rekodi zinaonesha hadi vibonde Swansea na Burnley wamefunga magoliengi nyumbani kuliko Manchester United, Swansea wamefunga magoli 22 katika uwanja wao wa nyumbani, Burnley wamefunga magoli 23 katika uwanja wao wa nyumbani huku United wakifunga magoli 21 tu Old Trafford.
4.Msimu wa mwisho wa Ferguson unamsuta Mourinho. Ilikuwa mwaka 2012/2013 ambapo hadi kipindi kama hiki United wakiwa wamecheza michezo 30 walikuwa wamefunga mabao 70, lakini msimu huu hadi sasa Manchester United wamefunga mabao 46 tu.
5.Manchester United vs BurnleyMchezo kati ya Manchester United dhidi ya Burnley mwezi October mwaka ulikuwa na rekodi ya mashuti, katika mchezo huo United walipiga mashuti 38. Lakini hadi mchezo huo unakwisha Manchester United hawakupata bao hata moja na mchezo kuisha kwa sare ya bila bila.

0 comments:
Post a Comment