Msimu uliopita alipojiunga na Chelsea tu mara paap akawapa ubingwa wa Epl, yaani msimu wake wa kwanza Epl akaja na kombe, huyo ndio Tactic Master Antonio Conte ambaye sasa ameweka rekodi mpya, rekodi ambayo inaletwa na michezo 100 ya mwisho yeye kama kocha(popote).
Antonio Conte ndio kocha ambaye katika michezo 100 iliyopita katika ligi kubwa barani Ulaya ndiyo kocha aliyefanya vizuri kuliko kocha mwingine yoyote barani Ulaya, amevuna alama 243 katika michezo 100 iliyopita247, akishinda 79, suluhu 20 na kupigwa 11.
Anayemfuatia Conte ni kocha wa Juventus ya Italia Massimilano Allegri ambaye ameweka alama 238 katika michezo 100, huku Carlo Anceloti akishika nafasi ya 3 kwa kubeba points 236 katika michezo 100 iliyopita.
Kwa nchini Uingereza anayemfuatia Conte ni kocha wa Manchester City Pep Gurdiola ambaye katika michezo 100 iliyopita ameshinda michezo 72, suluhu 15, akapoteza michezo 13 na hivyo kuambulia alama 231 huku barani Ulaya akiwa nafasi ya 4.
Chini ya Gurdiola yupo Diego Simeone nafasi ya 5 ambaye amepata alama 214, Arsene Wenger anakuwa kocha wa tatu nchini Uingereza na huyu alama zote amezipata akiwa na timu moja huku akiwa wa 6 barani Ulaya,amabapo katika michezo yake 100 iliyopita alipata alama 197 akishinda mara 59, suluhu 20 na vipigo 21.
Marcio Pochettino anashika nafasi ya 4 Uingereza na ya 7 Ulaya kwani yeye ameshinda michezo 57, suluhu 26 akipigwa mara 17 na ana alama 197, akifuatiwa na Jose Mourinho nafasi ya 5 Uingereza.
Jose Mourinho ameshinda michezo 52, amesuluhu 29 na kupoteza 18 ambapo amepata alama 188, huku Jurgen Klopp akiwa nafasi ya 6 Uingereza na 10 barani Ulaya kwa ushindi mara 48, suluhu 27 na vipigo 25 akiambulia alama 171, kwa ujumla katika ligi ya Epl msimamo wa makocha waliofanga vyema mechi zao 100 zilizopita ni.
1.Antonio Conte
2.Pep Gurdiola
3.Arsene Wenger
4.Maurcio Pochettino
5.Jose Mourinho
6.Jurgen Klopp


0 comments:
Post a Comment