Mourinho kajibu kwa nini alimuacha Herrera vs Basel


Kocha wa Man United Jose Mourinho ambaye usiku wa September 12 2017 aliiongoza Man United katika mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Basel na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, ameamua kuweka wazi kwa nini hakumtumia Ander Herrera.
Ander Herrera alicheza game yake ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu England weekend iliyomalizika Man United ikiambulia sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City lakini kiungo huyo aliachwa katika mchezo wa jana wa Champions League dhidi ya Basel.
Pogba
Jose Mourinho ameweka wazi kuwa maamuzi yake hayo yalikuwa ya kiufundi wala hakuna sababu nyingine kwa sababu aliamua kutumia viungo wawili MaticPogba na Herrera kumuacha.
Herrera
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment