Yaliyomkuta Morata yamgeukia Romelu Lukaku, awaambia mashabiki wa United “tuheshimiane”

Katika wimbo mmbaya ambao huwezi hata kuuandika ni wimbo wa mashabiki wa Manchester United kuhusu mshambuliaji wao Romelu Lukaku, ni kati ya nyimbo ambazo zimekosa heshima.
Wimbo huo umekuwa maarufu sana katika siku za usoni ambapo mwanzo ulikuwa unaimbwa na kikundi kidogo tu cha mashabiki lakini baadae wimbo huo umezagaa kwa mashabiki wengi wa Manchester United.
Wimbo wa mashabiki wa Manchester United umekuwa ukiimbwa huku wakitaja maungo ya siri ya mwanasoka huyo yalivyo, jambo ambalo limetafsiriwa vibaya na watu wengi japo United wanaliimba kwa sifa.
Tayari chama cha soka nchini Uingereza FA kikeshaionya Manchester United kuhusu wimbo huu na kuitaka klabu hiyo kutafuta namna kuona ni kwa jinsi gani wanaweza wakawacontrol mashabiki zao.
Romelu Lukaku naye anaonekana kuchoka na sasa anaomba heshima itawale kati yake na mashabiki “ni faraja ninavyoungwa mkono na mashabiki wa Manchester United na nyimbo zao #Tuheshimiane” aliandika Lukaku.
Manchester United imeshawaonya mashabiki kuhusu jambo hilo. Kama unakumbuka wiki kadhaa zilizopita mshambuliaji wa Chelsea Morata alionekana kutofurahishwa na nyimbo za mashabiki wa Chelsea kuhusu yeye.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment